Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:06

Somalia Watafakari Jinsi ya Kufanya Uchaguzi Mwakani


Viongozi wa kitaifa na kikanda nchini Somalia wamemaliza siku tatu za mazungumzo katika mji mkuu wa Mogadishu juu ya njia bora ya kufanya uchaguzi mwaka 2016.

Viongozi hao wameamua kuvunja serikali inayotawala sasa mwezi Septemba mwakani lakini hawakuweka marufuku kwa Rais Hassan Sheikh Mahamud na wabunge 275 kugombea tena nyadhifa zao.

Bunge pia limeamua muundo wa uchaguzi ujao nakudai utalingana na mchakato wa wilaya na koo.

Muafaka huo umekuja kwa sababu mikoa mikuu katika nchi hiyo imegawanyika katika jukumu la kufanikisha kuchagua wabunge kutoka kwa wazee wa koo ama wawakilishi wa wilaya.

Serikali ya kwanza ya Somalia baada ya vita iliyochukuwa muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe ilichaguliwa na wazee 135 wa koo ambao walikutana mjini Mogadishu mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG