Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:58

Al-Shabab Washukiwa Kushambulia Pwani ya Kenya


Washambuliaji waliokuwa na silaha wanaosadikiwa ni wafuasi wa kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia wamewaua watu kadhaa pwani ya Kenya.

Watu walouwawa walikuwa katika gari aina ya Canter wakiwasafiri kutoka Mombasa kwenda kaunti ya Lamu katika eneo la Kinumbi kilometa chache kutoka eneo la Mpeketoni.

Kwa mujibu wa idara ya polisi mjini Mombasa juhudi zinaendelea kuwatafuta washambuliaji.

Pia imesema katika barabara hiyo ya Mpeketoni kuelekea Mkowe gari la maafisa wa polisi nao limetekwa nyara na washambuliaji hao walilikimbiza gari katika msitu uliokuwa karibu.

Pia imeongeza kuwa kwa vile karibu na eneo hilo la tukio kuna kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (GSU) walifuatilia na walipofika ndani ya msitu huo walifanikiwa kupata gari hilo.

Pamoja na kufanikiwa kulipata gari hilo polisi walikuta likiwa limeteketea kabisa na haijulikani kama maafisa hao wa polisi wamechomwa ndani ya gari au la.

Katika taarifa za awali zilizotolewa na kamanda wa polisi katika eneo la pwani, Francis Wanjohi ni kwamba jeshi la polisi linafanya kila juhudi kuwasaka na kuwatia mbaroni washambuliaji na kuahidi kuwa watapatikana.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG