Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 02:18

Wanawake Watarajiwa Kushinda Uchaguzi Saudi Arabia


Karibu wanawake 13 wameshinda viti katika uchaguzi wa baraza la manispaa nchini Saudi Arabia.

Uchaguzi huo unakuwa wa kwanza wa wazi kwa wapiga kura na wagombea wanawake.

Matokeo ya awali ya Jumapili yanaonyesha Salma bint Hizab al-Oteibi alikuwa mwanamke wa kwanza kuthibitishwa mshindi kwa wanawake wanaowania viti katika baraza la manispaa.

Al-Oteibi amewashinda wanaume saba na wanawake wengine wawili katika nafasi hiyo mjini Madrakah karibu kilometa 150 kaskazini mwa Maka.

Mitandao yenye uhusiano na serikali na mashirika ya habari ya kujitegemea yameashiria kuwa wananchi wa Saudi Arabia wamechagua karibu wanawake 17.

Matokeo ya mwisho bado hayaja tangazwa ili kujua majumuisho kamili ya uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG