Upatikanaji viungo

Wafanyabiashara wagoma Kampala


FILE -wachuuzi wakiwa katika mgomo wa zamani mjini Kampala, Uganda.

Na Kennes Bwire

Shughuli za biashara zimekwama jijini Kampala nchini Uganda, maduka na masoko yote yakiwa yamefungwa kufuatia mgomo wa wafanyabiashara.

Wafanyabiashara wanagoma wakilalamikia mwelekeo wa mamlaka ya ushuru URA wa kutaka wafanyabiashara watakaopatikana na dosari za malipo ya ushuru kukamatwa na kupelekwa jela moja kwa moja na kutoachiliwa kwa dhamana wakati kesi inaposikilizwa.

Makala pia wanaunga mkono mgomo wa wafanya biashara hao, hali ambayo imesababishwa na utaratibu unaotatiza wafanya biashara kwa muda mrefu. Usafirishaji bidhaa kutoka bandari za Mombasa, Kenya, na Dar es salaam, Tanzania pia umezorota kutokana na msimamo huo wa wafanya biashara.

XS
SM
MD
LG