Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:27

Kura Kuanza Kuhesabiwa Burkina Faso


Raia wa Burkina Faso akishiriki uchaguzi wa Jumapili
Raia wa Burkina Faso akishiriki uchaguzi wa Jumapili

Wapiga kura nchini Burkina Faso wamepiga kura hapo Jumapili kwa ajili ya kumchagua rais mpya na Bunge.

Uchaguzi huo umeitwa wa wazi kuliko chaguzi zote katika historia ya nchini hiyo.

Watu milioni 5 waliojiandikisha walikuwa na haki ya kumchagua mmoja kati ya wagombea urais 14.

Saa 12 za kupiga kura zilimalizika saa kumi na mbili kwa saa za huko siku ya Jumapili, na maofisa walianza kuhesabu kura.

Matokeo ya kwanza yanatarajiwa kuanza kutolewa Jumatatu kutoa uelekeo wa uchaguzi huo kwa hatua ijayo.

Kama hakuna atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura, duru ya pili ya uchaguzi itafanyika ili kupata mshindi.

Rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaore aliiongoza nchi hiyo kwa miaka 27.

Bwana Compaore mwaka jana alijaribu kuondoa kipengele katika katiba cha muda maalum wa rais kuhudumu na kutaka kuendelea kubaki madarakani.

Hatua hiyo ilizua maadamano yaliyomfanya Rais huyo ajiuluzu wadhifa wake.

XS
SM
MD
LG