Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 10:49

Papa Ataka Wanaopigana Afrika ya Kati Kuacha


Papa Francis akisalimia watoto alipofika nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Papa Francis amezitaka pande zote zinazopingana nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati kuweka silaha zao chini kuunga mkono juhudi za kumaliza mzozo wa kimadhehebu.

Baba mtakatifu aliwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui Jumapili kwa ajili ya kuhamasisha amani katika nchi iliyo katika mgogoro wa kisiasa na mapigano baina ya wanamgambo wa Kikristo na Kislamu.

Akihutubia umma katika kanisa kuu la Bangui, Papa Francis amewasihi wale wote wanaopigana kwa maneno yake amesema “waweke chini silaha hizi zinazoangamiza uhai.”

Mapema Baba mtakatifu alitaka uwepo wa umoja na watu kutoruhusu tofauti zao za kidini kuwagawa.

Katika matamshi yake akiwa katika ikulu ya Bagui, amesema ana matumaini uchaguzi ujao utawezesha nchi hiyo kuingia katika ukurasa mpya wa historia.

XS
SM
MD
LG