Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:41

Papa Francis awasili Kenya


Baba mtakatifu Francis amewasili nchini Kenya na kupitia ukurasa wake wa Twitter, Papa Francis aliandika kwa lugha ya Kiswahili "Mungu abariki Kenya! God bless Kenya."

Kuwasili kwake kunakuwa ni kuanza kwa ziara yake ya barani Afrika Jumatano katika vituo vilivyopangwa vya Kenya, Uganda na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Baada ya kuwasili mjini Nairobi leo, papa atakutana na Rais Uhuru Kenyatta na kundi la Wanadiplomasia huko Ikulu.

Hapo kesho atakutana na kundi la watu wenye imani tofauti katika ubalozi wa Vatican katika mji mkuu wa Kenya.

Baadaye atafanya misa katika chuo kikuu cha Nairobi.

Siku ya Ijumaa papa atatembelea watu masikini mjini Nairobi katika eneo la Kangemi na kukutana na vijana katika uwanja wa Kasarani.

Katika vituo vya baadaye amepanga kutembelea sehemu ya mashahidi watakatifu nchini Uganda na kutembelea Msikiti na kambi ya wakimbizi huko Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Katika ziara yake Baba Mtakatifu anatarajiwa kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa, na migogoro baina ya makundi ya kidini pia inatarajiwa kujadiliwa wakati wa ziara yake.

XS
SM
MD
LG