Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:40

Museveni Aonywa kwa Barua


Tume ya uchaguzi nchini Uganda imemwandikia barua mkuu wa polisi na nakala yake kupewa Rais Yoweri Museveni na chama chake cha NRM.
Taarifa zinasema nakala nyingine imetumwa kwa kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ICC.
Madhumuni ya barua hiyo ni kutaka dhuluma zinazodaiwa kufanyiwa kambi yake mgombezi wa urais Amama Mbabazi kuchunguzwa na ripoti kutolewa haraka iwezekanavyo.
Barua hiyo imeandikwa baada ya tukio la Helicopter iliyokuwa imepambwa picha zake Rais Museveni kutua katika mkutano wa Mbabazi.
Vilevile inatokana na mmoja wa meneja wa kampeni za Mbabazi kuuwawa siku ya jumamosi katika mazingira tatanishi.
Na huku Rais Museveni akiandikiwa barua, Bwana Mbabazi ametishia kufichua siri za serikali ya Museveni iwapo ataendelea kudhulumiwa.
Kwa zaidi unaweza kusikiliza ripoti ya mwandishi wetu wa Kampala Kennes Bwire.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG