Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 12:50

Tanzania Yapata Spika mpya wa Bunge


Zimbabwe Cabinet

Bunge la 11 la Tanzania limeanza kikao chake mjini Dodoma kwa kufanya uchaguzi wa spika wa bunge la kwanza katika awamu ya tano baada ya kukamilika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 na kumchagua mbunge wa Kongwa Job Ndugai.

Uchaguzi wa spika ulijumuisha wagombea wa vyama nane vya siasa vya CCM, CHADEMA, NRA, TLP, AFP, CCK na DP wakati mgombea kutoka chama cha CHAUMMA, kutotokea.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge, Bwana Job Ndugai alichaguliwa kwa kupata kura 254 kati ya kura 359 zilizopigwa

Mgombea huyo wa CCM alifuatiwa kwa kura na mgombea kutoka CHADEMA Goodluck Ole Medeye aliyepata kura 109 huku wagombea wa vyama vilivyobaki wengi wao wakikosa kura kabisa.

Bwana Ndugai ambaye katika bunge la kumi lililomalizika alikuwa Naibu Spika, alijinadi kuwa mzoefu wa kazi hiyo wakati wagombea hao walipopewa nafasi ya kujieleza kabla ya kuchaguliwa.

Baada ya uchaguzi huo wa spika Ndugai na baadaye kuapishwa , alianza kazi ya kuwaapisha wabunge wateule zoezi litakaloendelea mpaka alhamis wiki hii na baadaye kupata nafasi ya kuthibitisha jina la Waziri Mkuu litakaloletwa kwao na Rais wa Tanznaia, DK John Magufuli kabla ya kuhutubia Bunge Ijumaa wiki hii.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG