Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:46

Rais wa Nigeria kusaka fedha ziloporwa


Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amefanya kupambana na rushwa kuwa kipaumbele kwenye ajenda yake. Njia mojawapo ambayo rais Buhari anapanga kutekeleza hilo, ni kwa kufuatilia fedha zilizoibiwa kutoka kwa hazina ya serikali.

Kwa miaka kadhaa serikali za Nigeria zimeahidi kurudisha fedha zilizoibiwa kutoka kwa viongozi waliotangulia. Kwa mfano, utawala wa rais wa zamani Goodluck Jonathan , ulipata makubaliano ya kuwawezesha kurudisha fedha zilizochukuliwa na dikteta wa zamani marehemu Sani Abacha.

Na sasa serikali ya rais Buhari inasema kuwa imepata uungaji mkono kutoka kwa serikali za marekani na Ulaya, kusaka fedha zilizohamishwa kutoka Nigeria.

Rais Buhari hajaeleza bayana jinsi utawala upi anapanga kuuchunguza. Rais Buhari alishinda kura nyingi kutoka kwa watu waliokuwa na wasiwasi kuhusu rushwa iliyokuwepo chini ya mamlaka ya Bw. Jonathan.

Wakati Bw. Buhari alisema katika hotuba yake ya kuapishwa kwamba alikuwa haangalii kulipiza kisasi, lakini wachambuzi wanasema utawala wa bw. Jonathan huwenda ukalengwa katika uchunguzi wowote.

Rushwa kwa muda mrefu imekuwa ikitajwa kama mojawapo ya sababu kwa nini Wanigeria bado wako katika hali ya umaskini, licha ya taifa hilo kuzalisha mafuta mengi zaidi kuliko sehemu nyengine yeyote barani Africa.

Lakini hata juhudi za ngazi ya juu za kurudisha mali iiyoporwa, kama vile kupatikana kwa dola takriban millioni 380 zilizoibwa na Bw. Abacha. Bi. Idayat Hassan mkurugenzi wa kituo cha demokrasi na maendeleo anasema kwamba licha ya habari hizo zilizotangazwa mapema mwaka huu za kupatikana kwa fedha hizo,hakujawanufaisha Wanigeria.

Serikali ya rais Buhari inahitaji fedha zote itakazoweza kupata. Rais hivi karibuni alielezea kuwa hazina ya serikali inakaribia kuwa tupu. Wiki hii serikali ilisema itatumia accaounti maalum ya fedha za ziada zilizopatikana kutokana na mauzo ya mafuta kulipa madeni ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG