Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 10:27

Hussein Rajabu awataka wanasiasa kupigania mageuzi Burundi


Hussein Rajabu mwenyekiti wa chama tawala cha Burundi CNDD-FDD

Mwenyekiti wa zamani wa chama tawala cha Burundi CNDD-FDD, Hussein Rajabu ametowa wito kwa Warundi wenzake kuacha kupigania madaraka na badala yake kujaribu kushirikiana kuleta mageuzi ya kidemokrasia.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kutoka jela hapo Marchi 2, 2015, Bw Rajabu akiwa mafichoni anasema ametoka wakati huu kutokana na msaada na wenzake wa pande zote.

Hussein Rajabu azungumzia malengo yake ya kisiasa na VOA
please wait

No media source currently available

0:00 0:11:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

"Sasa kwa hivyo wote wameona wakati umewaadia lakini hakuna hata mmoja anathubuti kusema ukweli wa yale walokwisha yapanga katika chama cha CNDD-FDD. Kila mmoja alikua anakaa kimya akishangiriya yale Rais Pierre Nkurunziza alikua anasema."

Mwanasiasa huyo mashuhuri anasema kiongozi wa Burundi yuko katika muhula wake wa pili, na kufuatana na makubaliano ya chama chao "hakuna mtawala yeyote anaeweza kuzidisha muda wa miaka 10, yani mihula miwili ya miaka mitano - mitano."

Bw Rajabu amewasihi wanasiasa wa Burundi kuacha kupigania uwongozi na badala yake wapiganie mageuzi nchini. Anasema miungano ya kisiasa haina uthabati, na hivyo ni muhimu kwa Warundi kuungana pamoja ili kuondowa kikundi kinachotaka kuendesha taifa la Burundi kinyume cha demokrasia.

XS
SM
MD
LG