Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 16:27

Marekani na washirika washambilia Islamic State


Picha ya maktaba:

Wakati majeshi ya Iraq, yakisonga mbele kuukomboa mji wa Tikrit, kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State, muungano unaongozwa na Marekani umeendelea na kampeni ya mashambulizi ya anga.

Mashambulizi hayo yanafanywa kwa wanamgambo hao nchini Syria, na Iraq, kwa mashambulizi ya anga 13 yakilenga zaidi karibu na Kobani, na Fallujah.

Msemaji wa Pentagon, Kanali Steve Warren, amesema kwamba Marekani na washirika wake wamefanya karibu mashambulizi ya anga 2,800 toka kuanza kwa kampeni mwezi Agasti.

Mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika, Dilshad Anwar, aliona uthibitisho wa mashambulizi makali ya anga katika eneo la Kirkur.

Maafisa wa ulinzi wa Marekani wamesema eneo hilo lilishambuliwa mara mbili na muungano huo katika siku ya mwisho.

XS
SM
MD
LG