Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:56

Ndege itayotumia nguvu ya jua yendelea na safari kuzunguka dunia


Ndege inayotumia nguvu za jua ikijiandaa kuondoka uwanja wa ndege wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, Jumatatu, Machi 9, 2015.
Ndege inayotumia nguvu za jua ikijiandaa kuondoka uwanja wa ndege wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, Jumatatu, Machi 9, 2015.

Ndege ya Uswis, inayotumia nguvu ya jua ilitua salama nchini Oman, baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya safari yake kuzunguka dunia bila kutumia mafuta.

Ndege hiyo ilitua Mascut, saa 10 tangu iliporuka kutoka Abu Dhabi.

Ndege hiyo iliyotengenezwa kwa kutumia kabon fiber ina kiti kimoja na mashine mbili zinazotumia nguvu ya jua.

Mabawa yake yana urefu wa mita 72 ambayo ni mapana zaidi ya mabawa ya ndege aina ya Boeing 747, na ina wa chini ya tani 2.5.

Vinasa mionzi vya jua 17,000 vimejengwa katika mabawa na kuweka akiba nguvu ya jua ili kuiwezesha kuruka wakati wa usiku.

Ndege hiyo ilichukuwa miaka 12 kutengenezwa na ilibuniwa na wanasayansi walili Bertrand Piccard, na Andre Borschberg.

XS
SM
MD
LG