Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:55

Hatuwa zatakiwa kuchukuliwa kuwalinda Wanahabari Wanawake


Picha ya maktaba ya kikao cha taasisi ya wanahabari barani Ulaya

Taasisi ya usalama na ushirikiano huko ulaya (OSCE) imetoa wito Ijumaa kuwa hatua za haraka zichukuliwe kupambana na ongezeko la vitisho na manyanyaso kwenye mtandao kwa waandishi wa habari wanawake.

Akizungumza huko Vienna, mwakilishi wa OSCE, anaehusika na uhuru wa vyombo vya habari, Dunja Mijatovic alisema vitendo kama hivyo vina nia ya kumshushia hadhi mwandishi wa habari kama mwanamke badala ya kuzungumzia kilichomo katika makala.

Waandishi wa habari wanawake wamekuwa walengwa hasa katika ripoti za uhalifu, kisiasa na masuala nyeti ya kijamii ikiwemo miiko na maadili mengine katika jamii ya leo.

Mijatovic aliwasilisha mapendekezo kwa nchi zilizoshiriki kwenye OSCE ili kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuweka kipaumbele swala kuboresha idara za sheria na kuchangia kwa mazingira bora na yenye kuleta matumaini katika nyanja ya habari.

XS
SM
MD
LG