Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:25

Tunisia yashinda na kuongoza kundi B


Olympic Park Flags
Olympic Park Flags

Tunisia imejipatia ushindi wake wa kwanza katika michuano ya fainali za kombe la mataifa Afrika Alhamisi baada ya kutoka nyuma na kuifunga Zambia 2-1 katika mechi ya kusisimua ambayo ilikuwa na dalili za Zambia kushinda. Tunisia sasa inaoongoza kundi B ikiwa na pointi nne baada ya mechi mbili

Baada ya kukosakosa magoli kadha Zambia ilijipatia bao la kwanza katika dakika ya 59 baada ya Emmanuel Mayuka kuwachia mkwaju mkali kutoka nje kidogo ya penalti box baada ya kupokea pasi kutoka kwa Kalaba.

Lakini goli la Zambia lilidumu kwa dakika 10 tu kwani Akaichi alisawazisha katika dakika ya 69 kwa kuchomekea pasi pasi fupi wavuni. Bao hilo bila shaka liliwatetemesha Zambia kwani hadi hapo walikuwa wametawala mchezo lakini Tunisia ikapata nguvu mpya.

Kuanzia hapo Tunisia ilichachamaa na kujipatia bao la ushindi katika dakika ya 88 pale Chikhaoui alipogonga kichwa safi kutoka pasi ya Msakhi na kumwacha kipa wa Zambia Mweene akidaka hewa.

Zambia hawajashinda hata mechi moja ya kimataifa tangu kuchukua kombe hili 2012, lakini pia ni mara ya kwanza kushindwa katika mechi 13 za mashindano hayo.

XS
SM
MD
LG