Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:46

Uwanja wa ndege wa Nairobi umefungwa kufuatia moto mkubwa


Firefighters struggle to put out a fire at the Jomo Kenyatta International Airport in Kenya's capital Nairobi, August 7, 2013.
Firefighters struggle to put out a fire at the Jomo Kenyatta International Airport in Kenya's capital Nairobi, August 7, 2013.
Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema safari za ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi zitanaza baadae Jumatano baada ya moto mkali wakati wa alfajiri kuwalazimisha maafisa kuufunga uwanja huo.

rais Uhuru Kenyatta alitembelea uwanja huo mchana wa leo na katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Manoah Esipisu amesema safari za ndani ya nchi na za nedeg za mizigo zitanaza jioni ya Jumatano. hakuna taarifa iliyotolewa juu ya wakati gani safari za kimataifa zitakapoanza.

Haijajulikana bado sababu za moto huo ulozuka alfajiri ya Jumatano kwenye uwanja wa ndege mkubwa na muhimu kabisa wa Afrika Mashariki wa Jomo Kenyatta.

Mashahidi wanasema walishuhudia moto wa manjano ukipayuka kutoka eneo la kuwasili abiria huku wazima moto, wanajeshi na watu wa kawaida wakijaribu kuuzima moto huo.
hakuna mtu anaripotiwa kujeruhiwa. Uwanja wa ndege wa Nairobi ni moja wapo wa viwanja vya ndege vyenye shughuli nginyi Afrika Mashariki ukihudumia takriban wasafiri milioni tano kila mwaka.
XS
SM
MD
LG