Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 21:53

Angola yaanza kupiga kura za uchaguzi.


Mtu mmoja akipiga kura yake katika mji wa Luanda, Aogosti 31, 2012.
Mtu mmoja akipiga kura yake katika mji wa Luanda, Aogosti 31, 2012.
Raia milioni 9.7 wa Angola wanapiga kura za wabunge ijumaa ambapo pia watachagua Rais wan chi yao. Chama cha kiongozi aliyoko madarakani Jose Eduardo Dos Santos kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kushinda.

Siku chache zilizopita ziliandamwa na madai ya upinzani kwamba uchaguzi hautakuwa huru na wa haki.

Katika kampeni za mwisho mjini Luanda alhamisi, Rais Jose Eduado Dos Santos alionekana ana ujasiri wa kushinda.

Rais huyomwenye umri wa miaka 70 anatarajiwa kushinda uchaguzi huo na kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano licha ya mara nyingine kushutumiwa kwa rushwa. Amekuwa akitawala nchi hiyo tangu mwaka 1979.

Uchaguzi huu unaonekana kama hatua inayoweza kuwa muhimu kwa Angola ikiimarisha demokrasia na amani na kuendesha uchaguzi wake kwa amani.
XS
SM
MD
LG