Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:25

UNHCR :Matatizo ya kiafya yakumba wakimbizi Sudan


wakimbizi wa sudan
wakimbizi wa sudan
Maafisa wa Idara ya kuwahudumia wakimbizi ya Umoja wa Mataifa wamesema matatizo ya afya yanayosabaishwa na hali mbaya ya hewa na ukosefu wa huduma ya maji safi yanawakumba wakimbizi 170,000 wa-Sudan wanaoishi katika makambi na hifadhi kote katika majimbo ya Unity na Upper Nile ya Sudan Kusini.

Afisa mkuu wa afya wa UNHCR Dr. Paul Spiegel alielezea hali hiyo kama ya kushtua huku wakimbizi wengi wakisumbuliwa na maambukizo ya mapafu, kuharisha , malaria na kipindupindu magonjwa ambayo sasa ni tishio.

Msemaji wa idara hiyo Adrian Edwards aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa huko Geneva kwamba takriban nusu ya wakimbizi wa Upper Nile ni watoto wasio zidi umri wa miaka 11 na wengi mama zao au watu wanaowahudumia ni wagonjwa sana kuweza kuwahudumia.

Amesema karibu watoto 1600 walio chini ya umri wa miaka mitano wanautapia mlo mkubwa katika kambi ya Yusuf Batil inayohifadhi wakimbizi wa 34,000 wa Sudan kutoka jimbo la Blue Nile.
XS
SM
MD
LG