Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:25

Mwandishi wa habari wa Somalia auwawa


Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
Watu wenye silaha wamemuuwa mwandishi wa habari maarufu wa Somalia eneo ambalo limekuwa hatari kwa watu wenye taaluma hiyo duniani.

Watu wasiojulikana jana walimuuwa kwa risasi Yusuf Ali Osman anayejulikana sana kwa jina la farey katika wilaya ya dharkenely mjini Mogadishu .

Osman mkurugenzi wa zamani wa radio Mogadishu alikuwa anafanya kazi katika wizara ya habari ya somalia.

Jumuiya ya waandishi wa habari wa somalia iliyoko uhamishoni nchini Kenya imesema Osman ni mwandishi wa habari wa nane kuuwawa nchini somalia mwaka huu. katika taarifa jumuiya hiyo imesema inaumiza na kuvunja moyo kumpoteza mwandishi wa habari mahiri kila mwezi.

Mwakilishi maalumu wa umoja wa mataifa kwa ajili ya somalia Augustine Mahiga alilaani kuuwawa kwa Osman na kutoa mwito tena kwa maafisa wa somalia kufanya uchunguzi wa mashambulizi kwa waandishi wa habari.
XS
SM
MD
LG