Maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku 100 za mauaji ya kimbari yakiendelea huko Kigali, Rwanda. Picha zote kwa hisani ya Ikulu ya Kigali.
Wagombea kiti cha rais katika uchaguzi wa Disemba 20 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanazunguka nchi nzima kunadi siasa na sera zao kukiwepo na idadi kubwa ya wafuasi wanaojitokeza kwa mikutano yao.
Kura zinahesabiwa nchini Madagascar baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais ulosusiwa na idadi kubwa ya wapinzani. Uchaguzi umefanyika baada ya wiki kadhaa za ghasia na maandamano, na katika mji mkuu wa Antananarivo wafuatiliaji wanasema uchaguzi umefanyika kwa amani.
Maafisa wa afya wa Gaza wanasema ukosefu wa mafuta imesababisha kusitishwa kazi kwenye hospitali kadha Gaza kaskazini ambako watoto watano wachanga wamefariki Jumapili pamoja na wagonjwa 7 walokua mahtuti baada ya mashini za kuwapa oxygen kusita kufanya kazi.
Wataalam wanasema Hamas imetekeleza uhalifu wa kivita kwa kufanya mashambulizi holela ya roketi na shambulizi la Oktoba 7 dhidi ya Israel ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,400.
Mapigano yameongezeka huko Gaza, huku maandamano yakifanyika katika pembe zote za dunia kuunga mkono Palestina na kutaka kuachiliwa kwa mateka.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kukimbia kutoka makazi yao kaskazini mwa ukanda wa Gaza mwishoni mwa wiki hii tangu Israel kuanza mashambulio dhidi ya kundi la Hamas, huku Umoja wa Mataifa ukionya hali ni mbaya kabisa katikia ukanda huo.
Mapigano makali yameripotiwa kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas, siku ya pili baada ya wanamgambo hao kuishambulia Israel. Maandamano ya kuunga mkono pande zote mbili yamefayika katika miji mbali mbali ya dunia.
Huku Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likiendelea na vikao vyake Ijumaa, waandamanaji wakitaka kumalizika udhalimu kwa watu wa Sierra Lione.
Maandamano yafanyika kupinga serikali ya Iran kwa kile kinacho elezwa kuwa uvunjifu wa haki za binadamu.
Rais wa Kenya William Ruto, Jumatatu, amefungua mkutano wa kilele wa hali ya hewa barani Afrika na kuwaomba wajumbe waliohudhuria kutumia mkutano huo kusaidia kutoa mapendekezo ya Afrika kwenye mkutano ujao wa hali ya hewa wa COP28 utakaofanyika Dubai mwezi Novemba.
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fatah al-Burhan amekutana na mshirika wake mkuu rais Abdel Fatah al-Sisis siku ya Jumanne wakati wa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa mapigano mwezi April nchini mwake.
Pandisha zaidi