Milipuko ya mabomu yavuruga mbio za Boston Marathon
Milipuko ya mabomu yavuruga mbio za Boston Marathon
Milipuko miwli yatokea wakati wa mbio ndefu za Boston marathon
1/14Picha ya video ya kituo cha WBZ TV, ambapo watu na wanariadha wakikimbia kutoka mahala inayosemekana mabomu mawili yalilipuka moja baada ya nyingine. Aprili 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
2/14Wafanyakazi wa huduma za afya wakiwasaidia watu kwenye eneo la kumalizika mbiyo za Marathon ya Boston 2013. April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
3/14Wafanyakazi wa afya wakimbeba mtu aliyejeruhiwa upande wa pili wa tepu ya kumaliza mbiyo za Boston kufuatia mlipuko wa bomu. April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
4/14Mwanamke akiikumbatiwa na mwanamume anaemtuliza baada ya milipuko miwili karibu na hema ya huduma za dharura, Boston, Massachusetts, Aprili 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
5/14Wafanyakazi wa afya wanasukuma gari la mgonjwa wakimpeleka mtu aliyejeruhiwa kwenye eneo la hema ya huduma za dharura upande wa pili wa eneo la kumaliza mbio za Marathon za Boston. Aprili 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
6/14Wafanyakazi wa afya wanasukuma gari la mgonjwa wakimpeleka mwanamke aliyejeruhiwa kwenye eneo la hema ya huduma za dharura upande wa pili wa eneo la kumaliza mbio za Marathon za Boston. Aprili 15, 2013..
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
7/14Mkimbiaji wa Marathon asiyejulikana akiondoka kwenye mashindano akilia karibu na uwanja wa Copley baada ya milipuko huko Boston, Aprili 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
8/14Wafanyakazi wa huduma za afya wakiwasaidia watu baada ya mlipuko.April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
9/14Runner John Ounao crying when he finds friends after several explosions rocked the finish of the Boston Marathon, April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
10/14A runner in a wheelchair is taken from a triage tent after explosions went off at the 117th Boston Marathon in Boston, Massachusetts April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
11/14Moja wapo ya eneo la mlipuko kwenye barabara ya Boylston Street karibu na mahala ya kumaliza mbiyo za Marathon ya Boston, Aprili 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
12/14Polisi analinda eneo ambalo kuna hema ya huduma za dharura karibu na eneo ambalo mabomu yaluilipuka huko Boston, April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
13/14Justine Franco wa Montpelier, Vermont, akibeba bango lenye jina la rafiki yake April, kwenye uwanja wa Copley ambae alishiriki kwa mara ya kwanza mbiyo za Marathon ya Boston, April 15, 2013.
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
14/14Rais Barack Obama akiondoka kwenye jukwa baada ya kuzungumza kwenye chumba cha waandishi habari cha White House, April 15, 2013, kufuatia milipuko kwenye mbiyo za Marathon ya Boston
Watu watatu wameuwawa na takriban 100 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka karibu na eneo la kumaliza mbio za 117 za Boston marathon.
Previous slide
Next slide
Milipuko miwili ya mabomu iliyotokea karibu na mstari wa kumaliza mashindano ya mbio za Boston Marathon, nchini Marekani imewauwa watu wawili na zaidi ya 50 wengine walijeruhiwa Jumatatu.
Maafisa wa usalama walisema mlipuko wa tatu ulitokea kwenye maktaba ya John F.Kennedy iliopo katika mtaa mwingine wa Boston. Hakuna majeruhi yeyote aliyeripotiwa kutokana na mlipuko wa tatu na bado haijafahamika vyema kama mlipuko huo unahusiana na milipuko miwili iliyotokea awali kwenye mji huo.
Polisi wa Boston hawakusema kama milipuko ilikuwa sehemu ya shambulizi la ugaidi. Msemaji wa polisi alisema timu ya wataalamu wa kutegua mabomu walikuwa wakichunguza mifuko na vifurushi vilivyoachwa kiholela kwenye tukio la milipuko ya awali lakini hakuna vifaa vingine vyovyote vinavyohusiana na milipuko vilivyopatikana.
Picha za televisheni zilionesha matukio ya kuogopesha, mtaa ulijaa vifusi na damu, wafanyakazi wa huduma za dharura wakiwa wamebeba machela waliwasili mara moja kwenye mahala uharibifu mkubwa ulipotokea.
Milipuko ilitokea mmoja baada ya mwingine ikipishana sekunde chache tu karibu na eneo la kumaliza mashindano ya mbio ambayo yaliwashirikisha wanamichezo wapatao 27,000. Mashindano yalisitishwa baada ya milipuko kutokea pamoja na usafiri wa njia ya metro katika eneo hilo.
Rais Barack Obama amelihutubia taifa na kutoa rambi rambi zake kwa waathiriwa akiahidi kwamba wahusika wa tukio hilo watapatikana, watafikishwa mbele ya sheria na watafahamu kwa nini wamefanya kitendo hicho kiovu.
Wakati huo huo polisi nchini Ungereza wanasema wanatathmini mipango ya usalama kwa ajili ya mbio za marathon zitakazofanyika Jumapili mjini London, baada ya milipuko ya mabomu kutokea huko Boston na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wawili.
Waandaaji wa marathon mjini London wanasema wamewasiliana na polisi kuzungumzia mipango ya usalama mara tu waliposikia tukio la milipuko la Boston nchini Marekani.
Maelfu ya wanariadha wamepangiwa kushindana katika mbio za London Marathon, zitakazofanyika chini ya muda wa wiki moja.