Jumapili, Februari 07, 2016 Local time: 13:23

  Habari

  Kimbunga Sandy kuleta madhara Marekani

  Mike Strobel akijaza mchanga kwenye magunia kwa ajili ya kuweka kwenye eneo lake la biashara.
  Mike Strobel akijaza mchanga kwenye magunia kwa ajili ya kuweka kwenye eneo lake la biashara.
  Eneo la mashariki mwa Marekani linajiandaa kwa kile watabiri wa hali ya hewa wanabashiri kuwa kimbunga kikubwa kuliko vyote kupata kupiga katika eneo hilo.
  Kimbunga Sandy kinaelekea ufukwe wa Atlantic na kinatarajiwa kuungana na vimbunga vingine viwili kutoka kaskazini na kusababisha hali mbaya ya hewa itakayotanda kwa upana wa kilomita 1,200 na kuathiri wakazi milioni 60.

  Miji mikubwa imejiandaa kwa kimbunga hicho ikiwemo Washington, Baltimore,  New York , Philadelphia na Boston. Ilani zinatolewa kila mahali katike eneo la ufukwe wa mashariki ambapo kimbunga Sandy kinatarajiwa kupiga moja kwa moja kuanzia Jumatatu jioni.
  Kimbunga hicho tayari kina upepo wa kilometa 120 kwa saa huku spidi ya juu ikifikia kilometa 165 kutoka kati.

  Maafisa wanawaonya wakazi kuhakikisha wanayo maji ya kutosha ya kunywa, vyakula vya makopo na betri na kujiandaa kukaa siku kadhaa bila umeme.

  You May Like

  KATIKA PICHA: Kampeni za urais Marekani zaendelea New Hamphire

  Wanasiasa walio na azima ya kuwakilisha vyama viwili vikubwa vya kisiasa vya Marekani katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba mwaka huu waliendelea na kampeni zao katika jimbo la New Hampshire wikendi hii. Zaidi

  video Solar Innovation Provides Cheap, Clean Energy to Kenya Residents

  M-Kopa Solar is providing clean energy to more than 300,000 homes across East Africa by allowing customers to 'pay-as-you-go' via their cell phones Zaidi

  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.