Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 17:05

Kimbunga Haiyan cha sababisha vifo vya watu 10 000 Ufilipino


Meli iliyofikishwa nchi kavu juu ya nyumba zilizoharibiwa na mawimbi makubwa kutokana na kimbunga Haiyan Ufilipino. Nov. 10, 2013.
Meli iliyofikishwa nchi kavu juu ya nyumba zilizoharibiwa na mawimbi makubwa kutokana na kimbunga Haiyan Ufilipino. Nov. 10, 2013.
Wakazi walonusurika na kimbunga kikubwa kuwahi kutokea dunaini hadi sasa cha Haiyan, katikati ya Ufilipino wameanza kukata taama ya kupata msaada na hivyo wameanza kuiba katika maduka na misafara ya malori yanayowaletea msaada wa dharura.

Maafisa wa serikali wanasema wanaamini zaidi ya watu elfu 10 waliuwawa katika visiwa vya kati vya Leyte na Samar ambako kimbunga Haiyan kilifanya uharibifu mkubwa. wanasema wengi wa watu walifariki kwa kuzama wakati mawimbi yaliyokuwa makubwa sawa na ya tsunami kukumba visiwa hivyo.

Baada ya kutokuwa na chakula kwa siku tatu baadhi ya wakazi katika mji mkuu wa Leyte wa Tacloban walianza kupora maduka na nyumba katika mji huo ulokuwa na wakazi laki mbili.

Rais wa Benigno Aquino alitembelea Taclobana Jumapili na kusema kipaumbele cha serikali yake ni kuwasilisha msaada wa dharura na huduma za afya kwa walonusurika na kurudisha umeme na mawasiliano.

Idara za hali ya hewa zinasema kimbunga Haiyan kinatazamiwa kuwasili kaskazini ya Vietnam Juamtatu alfajiri baada ya kusababisha mvua nyingi katika kisiwa cha kusini cha China cha Hainan siku ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG