Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 02:36

Wizara ya mambo ya nje Marekani yatoa ripoti yake ya kila mwaka ya nchi kuhusu haki za binadamu


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza muhtasari kuhusu Ripoti za nchi kwa mwaka 2023 zilizotolewa hivi karibuni kuhusu Haki za binadamu , Jumatatu, Aprili 22, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza muhtasari kuhusu Ripoti za nchi kwa mwaka 2023 zilizotolewa hivi karibuni kuhusu Haki za binadamu , Jumatatu, Aprili 22, 2024.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani siku ya Jumatatu ilitoa ripoti zake za kila mwaka za nchi kuhusu haki za binadamu, ikielezea uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan na vita vya Israel-Hamas kama baadhi tu ya masuala makubwa ya haki za binadamu duniani.

Katika kukusanya ripoti hizi tumechukua kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, vya ukweli, ikiwa ni pamoja na kuripoti kutoka kwenye mashirika ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na vyombo vya habari, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alisema katika taarifa ya mtandaoni.

Mwaka ulioangaziwa na ripoti hizo 2023, uligongana na maadhimisho ya miaka 75 ya Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa. Ripoti hizo zinatokana na haki za binadamu zinazotambulika kimataifa zilizoainishwa katika tamko hilo, miongoni mwa makubaliano mengine.

Katika utangulizi wa ripoti hizo, Blinken alielezea kwanza uvamizi wa Russia nchini Ukraine kama ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Kupuuza na kudharau kwa haki za binadamu kwa Kremlinm kunaonyeshwa kikamilifu, alisema, akimaanisha matumizi yake ya vurugu kwa raia kama chombo cha vita.

Pia alizungumzia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kama tishio kubwa kwa haki za binadamu, akiongeza kuwa pande zote mbili katika mzozo huo zimesababisha ghasia za kutisha, vifo na uharibifu.

Forum

XS
SM
MD
LG