Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 16, 2024 Local time: 02:18

Wahamiaji kulipwa paundi 3,000, na Uingereza wakikubali kwenda Rwanda


Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa Keighley, Kaskazini mwa Uingereza Machi 8, 2024.
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa Keighley, Kaskazini mwa Uingereza Machi 8, 2024.

Serikali ya Uingereza inampango wa kuwalipa hadi paundi 3,000 kila muomba hifadhi nchini humo atakaekwenda Rwanda chini ya mpango wa hiari wa kusaidia kuondoa mrundikano wa wahamiaji ambao maombi yao bado yamekataliwa.

Makubaliano mapya na Rwanda ni tofauti na mpango ulokwama wa serikali, wa kuwaondoa kwa lazima karibu waomba hifadhi wote kwenda katika nchi hiyo ya Afrika ya mashariki, ambayo mwaka jana mahakama kuu iliamuwa inakwenda kinyume cha sheria.

Badala yake inafanana na sera iliyoko ya serikali , ambayo waomba hifadhi wanapewa msaada wa kifedha kuondoka Uingereza na kwende kwenye nchi zao, lakini chini ya sheria mpya watapewa pesa endapo watakubali kuishi Rwanda.

Kevin Hollinrake, waziri mdogo wa biashara amesema siku ya Jumatano sera mpya itatumia vizuri fedha za umma kwa kuwa ni rahisi kuliko kuwatunza watu wakiwa Uingereza ambako wamenyimwa hifadhi, lakini bado hawajaondolewa.

Kuna maelfu ya waomba hifadhi ambao maombi yao yamekataliwa, lakini hawawezi kuondolewa kwa sababu serikali hairuhusiwi kuwarudisha watu katika nchi iliyokumbwa na vita au yenye rekodi mbaya ya haki za binaadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG