Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 02:22

Wakimbizi Chad wako hatarini kukosa chakula – UN


Kambi ya Wakimbizi waliokimbia vita Sudan huko Adre Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP.
Kambi ya Wakimbizi waliokimbia vita Sudan huko Adre Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba kambi za wakimbizi zilizojaa watu Mashariki mwa Chad zinatarajiwa kuishiwa msaada na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu uliotokana na vita vya sudan.

Zaidi ya watu milioni moja Chad wakiwemo wakimbizi wanakabiliwa na hatari ya kutokua na chakula na msaada wa dharura, endapo misaada haitaongezwa, limesema Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa- WFP.

Katika kambi za wakimbizi huko Mashariki mwa Chad ukosefu wa maji safi ya kunywa na huduma za msingi za hifadhi ya maji taka zinasababisha kuenea kwa magonjwa hatari.

Maafisa wa Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF wamesema wamerekodi zaidi ya watu, 1,000 wenye ugonjwa Hepatitis E umeenea katika kambi zilizoko Mashariki mwa Chad ambao tayari umesababisha wanawake wajawazito kufariki.

Mratibu wa mungano wa mashirika ya misaada kwa ajili ya kanda hiyo Mraie Jose Alexander, amesema Ijumaa kuwa katika kambi ya Metche, ambayo inahifadhi wakimbizi 40,000, watu wako katika uhitaji mkubwa wa maji, chakula, makazi na huduma msingi za kuondoa uchafu.

Forum

XS
SM
MD
LG