Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 15:34

Wajumbe wa Hamas wapo Cairo kwa mazungumzo ya usitishaji mapigano Gaza


Majengo yaliyoharibiwa kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Hamas. April 16, 2024.
Majengo yaliyoharibiwa kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Hamas. April 16, 2024.

Matokeo ya leo yatakuwa tofauti. Tumefikia makubaliano juu ya masuala mengi, chanzo cha usalama cha Misri kimesema

Wajumbe wa Hamas waliwasili mjini Cairo Jumamosi kwa mazungumzo juu ya uwezekano wa kusitisha mapigano Gaza ambayo yatapelekea kurejeshwa Israel kwa baadhi ya mateka, afisa wa Hamas ameliambia shirika la habari la Reuters, huku mkurugenzi wa CIA akiwa tayari yuko diplomasia isiyo ya moja kwa moja.

Kituo cha televisheni cha Al-Qahera chenye uhusiano na serikali ya Misri pia kimethibitisha kuwasili kwa ujumbe wa Hamas mjini Cairo. “Matokeo ya leo yatakuwa tofauti. Tumefikia makubaliano juu ya masuala mengi, na machache yamebaki,” chanzo kimoja cha usalama cha Misri kiliiambia shirika la habari la Reuters.

Afisa wa Palestina mwenye kufahamu juhudi za upatanishi alionyesha matumaini ya tahadhari. “Mambo yanaonekana kuwa mazuri zaidi wakati huu lakini iwapo makubaliano yatafikiwa yatategemea ikiwa Israel imetoa kile kinachohitajika ili hilo litokee,” afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG