Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:37

Wafuatiliaji wa UN wachunguza vifo Syria


SYRIA
SYRIA

Watu zaidi ya 150 waliuawa katika kijiji cha Tremseh

Timu ya wafuatiliaji wa Umoja Mataifa nchini Syria imeondoka Damascus Jumamosi kuelekea katika eneo ambalo watu zaidi ya 150 waliuawa siku ya Alhamis, huku wanaharakati wa upinzani nchini humo wakiripoti mashambulizi mapya kwingineko nchini humo. Timu hiyo iliondoka mji mkuu wa Syria kuelekea kijiji cha Tremseh chenye wakulima wengi wa dhehebu la Sunni katika mkoa wa Hama. Nalo kundi la Syria na kutetea haki za binadamu limeiambia VOA kuwa majeshi ya serikali yanashambulia mji wa Khirbet Ghazaleh kusini mwa nchi Jumamosi. Kundi la upinzani linasema watu 31 wameuawa katika mashambulizi ya vikosi vya serikali kote nchini humo leo. Ijumaa,mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Kofi Annan alilaumu majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo waliojihami kwa silaha kwa mauaji katika kijiji cha Tremseh. Wanaharakati wa upinzani wanasema mashambulizi ya Alhamis ndiyo ghasia kubwa zaidi kufanywa kwa wakati mmoja tangu maandamano ya kupinga serikali ya Syria yaanze mwaka jana. Chombo rasmi cha habari huko Syria kililaumu magaidi kwa mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG