Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 13:13

Viongozi waendelea kuwasili kwa mazishi ya Fidel Castro


A man reads a newspaper in a street of Havana two days after Cuban revolutionary leader Fidel Castro died.
A man reads a newspaper in a street of Havana two days after Cuban revolutionary leader Fidel Castro died.

Viongozi kutoka mataifa yanayoegemea mrengo wa kushoto na yaliyo na ushirika na nchi ya Cuba, pamoja na wale wa mataifa mengine yanayoendelea, walianza kuwasili katika mji mkuu wa Cuba Havana siku ya Jumanne ili kuhudhuria ibada ya mazishi ya Fidel Castro, iliyopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Mapinduzi.

Castro aliongoza mapinduzi yaliyomweka madarakani mwaka 1959, na kulitawala taifa hilo kwa nusu karne. Rais huyo wa zamani aliyemkabidhi nduguye mdogo Raul Castro madaraka muongo mmoja uliopita kutokana na matatizo ya kiafia, alifariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 90.

Mataifa mengi ya Latin Amerika na Afrika yatamkumbuka Castro kama kiongozi aliepambana na ubeberu. Wengine wanamkumbuka kama liongozi wa kiimla alieharibu uchumi wa Cuba.

XS
SM
MD
LG