Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 03:02

Mabaki ya ndege ya EgyptAir 804 yaonekana baharini


Waziri wa usafiri wa anga wa Misri Sherif Fathi akizungumza na waandishi habari.
Waziri wa usafiri wa anga wa Misri Sherif Fathi akizungumza na waandishi habari.

Jeshi la Misri limesema Ijuma kua limepata mabaki ya ndege iliyoanguaka ya EgyptAir, karibu kilomita mia tatu kaskazini mwa mji wa Alexandria, kwenye bahari ya Mditerranean.

Msemaji wa kijeshi, Brigidia Jenerali Mohammed Samir, amesema kupitia ujumbe wa facebook leo Ijumaa kwamba mizigo ya abiria na mabaki ya ndege yalipatikana yakielea maji.

Makundi ya waokoaji yanaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo ambayo ilianguka baharini siku ya Alhamisi, ikielekea Cairo kutoka Paris, Ufaransa.

Mapema leo, wachunguzi wa kutoka Ufaranza wakiandamana na wataalam wa mitambo ya ndege aina ya Airbus waliwasili Cairo ili kusaidia na uchunguzi. Misri na Ugiriki zilituma ndege zake na vyombo vya majini kusaidia kutafuta mabaki ya ndege hiyo.

Timu kutoka Ufaransa zilitarajiwa kuungana nao huku Mrekani ikituma ndege ya kusaidia kwenye shughuli hiyo. Ndege hiyo ya EgyptAir iliyokuwa imebeba watu 66 ilipotea kwenye mawasilianao ya rada muda mfupi kabla ya kuingia kwenye anga ya Misri ikiwa kwa safari ambayo ingechukua masaa manne kutoka Paris hadi Cairo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa alipinga matamshi yaliyoenea kwamba ugaidi ulihusika, lakini anasisitiza kwamba wanafanya uchunguzi kujua sababu halisi ya kuanguka kwa ndege hiyo.

XS
SM
MD
LG