Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 16:53

White House yashinikizwa kufuta msaada kwa Malawi


Jengo la Bunge la Marekani, Washington DC
Jengo la Bunge la Marekani, Washington DC

Serikali ya Marekani yashinikizwa kusitisha msaada kwa Malawi baada ya nchi hiyo kumkaribisha Rais Omar al-Bashir wa Sudan

Mbunge mmoja wa Marekani anaishinikiza White House kusitisha mpango mkubwa wa msaada kwa Malawi, baada ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kumruhusu Rais wa Sudan, Omar al-Bashir kuitembelea.

Wakati wa mahojiano na Sauti ya Amerika, Idhaa ya Ki-ingereza hapo Jumatano, mbunge Frank Wolf, aliishutumu Malawi kwa kusaidia na kuunga mkono kile “kinachojulikana mhalifu wa vita.”

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa bwana Bashir kwa mashtaka ya uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki katika mkoa wa Darfur nchini Sudan.

Wolf alisema kama mwanachama wa ICC, serikali ya Malawi ilitakiwa kumkamata bwana Bashir, badala yake, kwa maneno yake mbunge huyo “kumtandikia zulia jekundu” wakati wa mkutano wa kieneo wiki iliyopita.

Mbunge huyo wa chama cha Repuplican alituma barua kwa Rais Barack Obama wiki hii akiitaka Marekani ifute msaada wa miaka mitano wa dola milioni 350 kwa Malawi.

Msaada huo uliidhinishwa mwezi April na Millennium Challenge Corporation, idara ya serikali ya Marekani ambayo inashirikiana na nchi maskini ambazo zinaonyesha nia ya dhati kwa utawala bora.

Wolf ni mwanachama wa wawakilishi bungeni katika kamati ambayo inashughulika na misaada ya serikali kuu. Mwezi Julai Millennium Challenge Corporation ilizuia msaada kwa Malawi, baada ya majeshi ya Malawi kufanya msako uliosababisha vifo kwa waandamanaji wanaoipinga serikali.

Waandamanaji waliandamana kupinga uhaba wa mafuta, ongezeko la bei na kutokuwepo uhuru wa haki za kiraia. Waandishi wa habari walipigwa na vyombo vya habari vya ndani vilizuiwa kuripoti ghasia hizo. Idara ya Marekani ilisema inatathmini kama isitishe au kufuta msaada wake kwa Malawi.





XS
SM
MD
LG