Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 02:05

Uingereza yasema Russia imehamisha mifumo yake ya ulinzi wa anga


Ndege za kivita za MiG-29 zikifanya maonyesho katika onyesho la Kimataifa la Ulinzi wa Wanamaji katika kituo cha Jeshi la Wanamaji la Kronstadt, nje ya St.Petersburg, Russia, Juni 21, 2023. (AP).
Ndege za kivita za MiG-29 zikifanya maonyesho katika onyesho la Kimataifa la Ulinzi wa Wanamaji katika kituo cha Jeshi la Wanamaji la Kronstadt, nje ya St.Petersburg, Russia, Juni 21, 2023. (AP).

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika taarifa yake ya kila siku ya kijasusi kuhusu Ukraine kwamba harakati za hivi karibuni za usafiri za Russia zinaonyesha kwamba Russia imehamisha mifumo yake ya kimkakati ya ulinzi wa anga kutoka kwenye  pwani yake ya Baltic ya Kaliningrad.

Hatua hii kutoka Kaliningrad ambayo imezungukwa pande tatu na nchi wanachama wa NATO inaangazia athari ya vita vya muda mrefu iliyotokana na baadhi ya vifaa muhimu vya kisasa vya Russia.

Jumamosi ilikuwa Siku ya Ukumbusho wa Holodomor huko Ukraine, wakati ambapo Waukraine wanakumbuka njaa iliyosababisha mamilioni ya watu kufariki dunia katika miaka ya 1930 kwa sababu ya sera za enzi ya Sovieti.

Holodomor ambayo ina maana kifo kutokana na njaa kwa lugha ya Ukraine ilikuwa sera ya makusudi ya Josef Stalin ambayo watu wa Ukraine, pamoja na zaidi ya nchi 30, wanaitambua kama mauaji ya kimbari lakini Moscow inakanusha.

Forum

XS
SM
MD
LG