Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 20:55

Uganda: Simba wapungua kwa asilimia 45


Ramani hii inaonyesha mbuga ya wanyamapori ya Queen Elisabeth nchini Uganda
Ramani hii inaonyesha mbuga ya wanyamapori ya Queen Elisabeth nchini Uganda

Uganda inakabiliwa na upungufu mkubwa wa idadi ya simba kufuatia kupungua kwa asilimia 45 kwa wanyama hao katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, wizara ya utalii na wanyamapori ilisema Jumanne.

Idadi ya simba ilipungua kutoka 493 hadi 275, kutokana kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa mzozo kati ya binadamu na wanyamapori, wizara hiyo ilisema.

“Simba walipingua sana kutokana na mauaji ya kulipiza kisasi, yanayosababishwa na mzozo kati ya binadamu na wanyamapori,” waziri Tom Butime alisema alipokuwa akitoa ripoti ya utalii nchini humo.

“Idadi ya simba ilipungua kutoka 493 mwaka 2014 hadi simba 275 mwaka 2023.”

Hata hivyo, Butime alisema anafuraha kutangaza kwamba idadi ya baadhi ya viumbe imeongezeka, wakiwemo sokwe, ambao idadi ilitoka 302 mwanzoni mwa mwaka wa 2000 hadi 452 ifikapo 2022.

Uganda ina sifa ya kuwa moja ya nchi yenye viumbe vingi hai duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG