Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 17:32

Trump Alaani Chuki Dhidi ya Wayahudi Iliyosambaa Marekani


Rais Donald Trump akiwa katika Makumbusho ya Kitaifa ya Historia ya Waafrika Weusi na Utamaduni wao, katika uwanja maarufu wa National Mall.
Rais Donald Trump akiwa katika Makumbusho ya Kitaifa ya Historia ya Waafrika Weusi na Utamaduni wao, katika uwanja maarufu wa National Mall.

Rais Donald Trump amelaani kuendelea kuwepo kwa tishio jipya la vitendo na kauli za chuki dhidi ya Wayahudi lililoenea nchi nzima, akisema ni lazima hao “waache hilo.”

Tishio hilo ambalo linawalenga jumuiya ya Wayahudi na vituo vyao ni lakutisha, linatia uchungu na ni lenye kusikitisha sana, hasa likitukumbusha kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu kuondokosha chuki, ubaguzi na maovu,” amesema Trump.

Kauli ya Trump ameitoa wakati akitembelea Jumanne, Makumbusho ya Kitaifa ya Historia ya Waafrika Weusi na Utamaduni wao, katika uwanja maarufu wa National Mall.

Kauli ya Rais inayolaani mashambulizi ya kauli na vitendo vya chuki yanayoelekezwa kwa wayahudi imetolewa siku moja baada ya umoja unaopambana na udhalilishaji (ADL) ulipotoa taarifa kuwa sio chini ya wayahudi 10 kutoka katika kituo cha jumuiya yao, katika majimbo mengi, yalipokea vitisho vya mabomu Jumatatu, ikiwa ni mtiririko wa nne wa vitisho hivi tangia mwaka uanze.

Hata hivyo umoja wa ADL umesema hakuna mabomu yaliyopatikana katika vituo hivyo na kueleza kuwa tishio hilo “lilikuwa ni kitisho tu.”

Wiki iliyopita, makaburi zaidi ya 170 ya Wayahudi yaliharibiwa katika eneo lao lilioko Chuo Kikuu cha Missouri.

ADL Jumatatu imeitaka tena serikali ya Trump kutengeneza mpango ambao utakabiliana na kile kinachoaminika kuwa ni kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya wayahudi wanaoishi Marekani.

Huko Washington wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatano iliyopita akiwa na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, Trump aliulizwa kuhusu matukio ya chuki dhidi ya wayahudi yanavyo ongezeka kote nchini Marekani.

Badala ya kulaani vitendo hivyo, Trump alizungumzia mafanikio yake ya kura za wajumbe katika “Electoral College,” na kulielezea kuwa suali aliloulizwa halijamtendea haki, akisababisha kukosolewa zaidi kwa kuwa kimya hata baada ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya wayahudi Marekani.

Mapema Jumatatu, hasimu wa Trump katika uchaguzi wa Novemba, Hillary Clinton ambaye ni Mdemokrati alikuwa amemtaka rais kuchukua hatua kali dhidi ya chuki hiyo.

XS
SM
MD
LG