Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:28

Takukuru yaanza kuchunguza TMAA, watendaji wa sekta ya madini Tanzania


د روژې د میاشتې رنګارنګ شیرینۍ
د روژې د میاشتې رنګارنګ شیرینۍ

Watendaji wote wanaodaiwa kuhusika katika sakata la kushindwa kudhibiti biashara ya kusafirisha mchanga wa dhahabu nje ya nchi, watachunguzwa na vyombo vya dola husika nchini Tanzania.

Serikali imesema watendaji ambao walihusika kwenye sakata hilo na sasa hivi hawapo madarakani au wanashikilia nyadhifa nyingine, nao lazima watahojiwa na taasisi hiyo ili kufahamu sababu ya kuruhusu taifa kupata hasara kubwa kiasi hicho.

Watendaji hao ni wanaofanya kazi Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Wizara ya Nishati na Madini na taasisi nyingine zinazohusika na madini.

“Kosa la jinai halina muda wala ukomo, wale ambao walikuwepo wizarani kitengo cha madini na kwa sasa hawapo nao tutawafuatilia,” alisema Mkurugenzi wa Taasis ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola.

Takukuru imesema itashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuchunguza suala hilo na watakaobainika kuhusika wote watashitakiwa.

Taarifa kutoka ndani ya TMAA zilisema Mtendaji Mkuu wa TMAA ambaye amesimamishwa kazi, Dominic Rwekaza aliripoti Takukuru Alhamisi.

“CEO hayupo ofisini, taarifa tulizo nazo yuko Takukuru,” alisema mmoja wa wasaidizi wake ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Kwa upande wake vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo amesema Rais Magufuli anaipenda nchi yake, angependa kila mwananchi afaidike na rasilimali za nchi, lakini inaonekana baadhi ya watendaji ambao wamepewa majukumu ya kusimamia na kulinda rasilimali hizo, wanaangalia maslahi binafsi.

Kuhusu kuunda kikosi kazi cha kushughulikia ulinzi wa rasilimali za nchi ikiwemo madini, Jenerali Mabeyo alisema tayari kipo na kinafanya kazi.

“Ila vyombo vya dola havipo kila eneo, tunachoomba kila mwananchi atusaidie kutupa taarifa za kiusalama,” alieleza Mkuu huyo wa JWTZ.

Msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema wameshaanza kutekeleza kazi waliyopewa na Rais Magufuli kuhusu ulinzi na kama kuna taarifa ambayo itahitajika kutolewa kwa umma watafanya hivyo. “Kwa sasa tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais,” alieleza Bulimba.

Baada ya kupokea ripoti ya ‘mchanga wa dhahabu’, Rais Magufuli aliagiza vyombo vya dola kuwachunguza Mtendaji Mkuu wa TMAA, Rwekaza na watendaji wengine wanaohusika na eneo hilo la usafirishaji makenikia Rais pia aliamuru watendaji wengine wachunguzwe na watakaobainika wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma za kuipa hasara Serikali.

XS
SM
MD
LG