Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 22:25

Serikali ya Marekani na CNSP kukutana kwa majadiliano ya uondoaji wa vikosi vya Marekani Niger


Mfuasi wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Nchi ya Niger (CNSP) akiwa ameshikilia bango linalosomeka "Anguka Ufaransa na Emanuel Gnacro, Hatutaki tena katika nchi yetu" wakati waandamanaji wanakusanyika nje ya Uwanja wa ndege wa Ufaransa huko Niamey mnamo Septemba 3, 2023.
Mfuasi wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Nchi ya Niger (CNSP) akiwa ameshikilia bango linalosomeka "Anguka Ufaransa na Emanuel Gnacro, Hatutaki tena katika nchi yetu" wakati waandamanaji wanakusanyika nje ya Uwanja wa ndege wa Ufaransa huko Niamey mnamo Septemba 3, 2023.

Serikali ya Marekani na baraza la Kitaifa la Kulinda Nchi huko Niger (CNSP), Balozi wa Marekani nchini Niger Kathleen Fitz Gibbon na Meja Jenerali Ken Ekman, Mkurugenzi wa Mikakati, Ushirikiano na Mipango wa Kamandi ya Marekani ya Afrika, watakutana na maafisa wa baraza hilo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Mathew Miller, amesema kwamba kama sehemu ya mazungumzo yanayoendelea ya serikali ya Marekani na Kamati ya Kitaifa ya Kulinda Nchi (CNSP), Balozi wa Marekani nchini Niger Kathleen Fitz Gibbon na Meja Jenerali Ken Ekman, Mkurugenzi wa Mikakati, Ushirikiano na Mipango wa Kamandi ya Marekani ya Afrika, watakutana na maafisa wa CNSP mjini Niamey hii leo ili kuanzisha majadiliano juu ya uondoaji kwa utaratibu na uwajibikaji wa vikosi vya Marekani kutoka Niger.

“Katika wiki ya Aprili 29, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Operesheni Maalum na Migogoro Christopher Maier na Luteni Jenerali Dag Anderson, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kikosi cha Pamoja watafanya mikutano ya kufuatilia huko Niamey kuratibu mchakato huo wa kujiondoa kwa uwazi. na kuheshimiana,” alisema Miller, katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Kurt M. Campbell atasafiri hadi Niamey katika miezi ijayo ili kujadili ushirikiano unaoendelea katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

“Marekani inathibitisha uungaji mkono wetu kwa watu wa Niger wanapopambana na ugaidi, kuendeleza uchumi wa nchi na kuelekea kwa utawala wa kidemokrasia,” alisema Miller.

Forum

XS
SM
MD
LG