Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:58

Salva Kiir amteua Machar makamu rais


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Riek Machar ni mwanaharakati wa miaka mingi aliyeshiriki katika vita vya ukombozi wa Sudan Kusini chini ya shujaa wa nchi hiyo John Garang

Rais wa nchi mpya ya Sudan Kusini Salva Kiir amemteuwa Riek Machar kuwa makamu rais wa nchi hiyo, na kuunda serikali ya muda.

Machar ambaye ameapishwa Jumatatu amekuwa akishikilia wadhifa huo katika serikali ya madaraka ya Sudan Kusini tangu kufariki kwa kiongozi wa ukombozi wa nchi hiyo John Garang.

Katika hatua nyingine Rais Kiir amechagua mawaziri kadha katika baraza lake jipya ambao wameelezewa kama mawaziri wa muda. Nhial Deng Nhial aliteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, Deng Alor atakuwa waziri wa mambo ya nje, na Pagan Amum ameteuliwa kuwa waziri atakeyeshughulikia utekelezaji wa mkataba wa amani wa 2005 ambao ulimaliza vita vya kusini na kaskazini.

Migogoro kuhusu mkataba huo imeongeza mivutano baina ya pande hizo mbili, ingawa serikali ya Khartoum imetambua uhuru wa Sudan Kusini.

Katika mahojiano Jumapili, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alidokeza kuwa atapigania jimbo lenye mgogoro la Abyei ambalo lina utajiri wa mafuta, ikiwa lazima. Lakini alisema pia anakaribisha jeshi la ulinzi wa amani kutoka Ethiopia katika jimbo hilo.

XS
SM
MD
LG