Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 02:32

Sakata la ubadhilifu wa fedha za umma laibua mjadala bungeni


Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe katikati akizungukwa na wananchi
Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe katikati akizungukwa na wananchi

Sakata hilo ambalo kwa sasa linachukua medani ya juu katika siasa za nchini Tanzania limeibuka tena bungeni alhamisi

Sakata la uchangishaji fedha lililoibua tuhuma dhidi ya katibu mkuu wa wizara ya madini nchini Tanzania ndani ya bunge limeibua mjadala mwingine wa namna ya mfumo wa matumizi ya fedha za Serikali unavyoendeshwa , huku katibu mkuu huyo akisimamishwa kazi tena kupisha uchunguzi wa kamati ya bunge.

Sakata hilo ambalo kwa sasa linachukua medani ya juu katika siasa za nchini Tanzania limeibuka tena bungeni alhamisi kwa baadhi ya wabunge kuhoji hatua zitakazochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo wa nishati na madini baada ya jumatano kuamriwa kurejeshwa tena kazini na alhamisi kusimamishwa kazi.

Freman Mbowe kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ndiye aliyeanzisha agenda hii wakati wa maswali ya papo kwa papo, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda. Bwana mbowe alihoji kama serikali haioni ni jambo muhimu kumpeleka tena likizo bwana David Jairo wakati kamati ya bunge inapofanya kazi yake, na ndipo waziri mkuu alipotoa ufafanuzi wa hatua ya Rais ya kumsimamisha tena kazi bwana Jairo.

Waziri mkuu alijibu akisema hatua imeshachukuliwa na Rais na itatoa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kubaini mazingira na mambo yote yanayoendana na mazingira yaliyojitokeza.

Wakati huo huo bwana mbowe pia aliibua hoja nyingine ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kuuliza kwamba pamoja na kuwa bunge litakuwa linachukunguza na kubaini makosa je serikali itaweza kuwachukulia hatua watakabainika kuwa wametumia vibaya fedha za umma.

XS
SM
MD
LG