Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:12

Rwanda yapiga kura ya maoni


Wananchi wa Rwanda wanaoishi Nairobi, Kenya wapiga kura mapema, Desemba 17, 2015.
Wananchi wa Rwanda wanaoishi Nairobi, Kenya wapiga kura mapema, Desemba 17, 2015.

Takriban wananchi milioni moja wanatarajiwa kupiga kura Ijumaa.

Na Sylivanus Karemera,

Kigali, Rwanda

Wananchi wa Rwanda wanaendelea na maandalizi ya kupiga kura ya maoni ili kumruhusu rais Paul Kagame kuendelea na madaraka baada ya mwaka 2017. Kura ya maoni ilipigwa Alhamisi na wananchi wa Rwanda waishio nchi za nje huku wale wanoishi ndani ya nchi hiyo wakitarajiwa kupiga kura Ijumaa.

Takriban wananchi milioni moja wanatarajiwa kushiriki kwenye zoezi hilo.

Hii inahitimisha miezi mine ya maandalizi ambapo wananchi kote nchini wenye haki ya kupiga kura wanatazamiwa kupiga kura hiyo ya maoni. Vituo vya kupigia kura vipatavyo 2800 vimetayarishwa ambapo wananchi wapatao milioni sita watashiriki.

Ni kura ambayo inatarajiwa kutokuwa na ushindani kutokana na jinsi wananchi waliovyoitikia kampeini za ‘ndiyo’.

Polisi wamesema kuwa kuna ulinzi na usalama na usalama wa kutosha.

Msemaji wa jeshi la polisi ACP Celestin Twahirwa amenukuliwa akisema kwamba maafisa wake wamejiandaa vilivyo.

“Kuna vituo zaidi ya 2800 kote nchini na tunatangaza kwamba kwenye maeneo hayo yote kutakuwa na usalama wa kutosha na polisi wamejiandaa kulinda usalama wa wapiga kura,’ alisema.​

Tume ya taifa ya uchaguzi imetangaza kwamba maandalizi yamekamilika na tayari wananchi kuanzia saa moja asubuhi siku ya Ijumaa watakuwa kwenye mistari ya kupiga kura ya maoni kwa ajili ya mabadiliko ya katiba.

Kura hii ni muhimu kwa ajili ya mabadiliko ya katiba ya Rwanda ambayo kama itapitishwa itamfanya Rais wa sasa Paul Kagame kugombea muhula mwingine wa tatu.Rais Kagame mwenyewe hajataangaza msimamo wake lakini baadhi ya mashirika na wakosoaji wamekosoa mkakati huo wa mabadiliko ya katiba.

XS
SM
MD
LG