Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 14:02

Russia na Marekani wana maslahi ya pamoja ya kuishinda Islamic State-Trump


 Trump akihojiwa na NBC Jumatano jioni huko New York.
Trump akihojiwa na NBC Jumatano jioni huko New York.

Mgombea kiti cha rais wa chama cha republican Donald Trump alimsifu rais wa Russia Vladmir Putin jumatano akisema kwamba amekuwa kiongozi bora kuliko rais wa Marekani Barack Obama.

Wakati wa kipindi maalum cha kituo cha televisheni cha NBC alichohudhuria baada ya minzani wake Hillary Clinton, kuhojiwa, Trump amesema anafikiri akiwa rais atakuwa na mahusiano mazuri sana na Putin. Pia akaongeza kwamba Russia na Marekani wana maslahi ya pamoja ya kulishinda kundi la Islamic State.

“Russia wantaka kuwashinda ISIS kwa kiasi kikubwa kama sisi Trump alisema, na kuhoji kwamba ikiwa wana uhusiano mzuri na Russia si itakua jambo rahisi kuwamaliza ISIS?

Pia alikosoa hatua za Marekani huko Iraq chini ya utawala wa Obama akisema Majenerali hawakufanikiwa akirudia tena msimamo wake kwamba Marekani ingeli kua imechukua udhibiti wa uzalishaji mafuta wa Iraq.

XS
SM
MD
LG