Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 14:07

Rais Ruto aiomba Afrika kutafuta ufumbuzi wa athari zinatokana na mabadiliko ya hali ya hewa


Rais wa Kenya William Ruto akiwahutubia wajumbe wakati wa wa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika (ACS) 2023 unaoendelea huko Nairobi, Kenya, Septemba 4, 2023. Picha na REUTERS/Moniah Mwangi
Rais wa Kenya William Ruto akiwahutubia wajumbe wakati wa wa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika (ACS) 2023 unaoendelea huko Nairobi, Kenya, Septemba 4, 2023. Picha na REUTERS/Moniah Mwangi

Rais wa Kenya William Ruto, amewaomba wajumbe wanaohudhuria mkutano wa kilele wa hali ya hewa barani Afrika kutumia mkutano huo kusaidia kutoa mapendekezo chanya ya Afrika yatakayopelekwa kwenye mkutano wa hali ya hewa duniani COP28 utakaofanyika Dubai mwezi Novemba.

Mkutano huo ambao unafanyika mjini Nairobi, unawajumuisha wakuu wa nchi, watunga sera, viongozi wa serikali, watoa maamuzi, wataalam wa mabadiliko ya hali ya hewa, mashirika ya kimataifa na mashirika ya kiraia, na sekta binafsi.

Katika hotuba yake kwa kikao cha ufunguzi Rais Ruto amesema wakati umefika kwa bara la Afrika kutafuta ufumbuzi wa athari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ruto amewataka wajumbe wa mkutano huo kutumia mkutano huo wa siku tatu kutathmini mitazamo, na kutafuta suluhu na kubuni mikakati ya kubadilisha utajiri wa rasilimali za Afrika kutoka kwa uwezo hadi kuwa fursa halisi, kwa kuelekeza uwekezaji mkubwa ambao utafanikisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, amekariri kuwa Afrika inaweza kuendesha mahitaji yake yote ya nishati kwa rasilimali zilizopo na lina uwezo wa kutosha wa kujitosheleza kabisa kwa mchanganyiko wa upepo, jua, jotoardhi, nishati ya uhakika, endelevu, na ya bei nafuu ya umeme wa maji.

Hatua chache kutoka ukumbi wa mkutano, wanaharakati wa mashirika ya kiraia wamekuwa wakifanya maandamano sambaba na mkutano huo, wakiomba kujumuishwa kwa jamii zilizoathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa. Wanaharakati wanadai kuwa ni mazoea ya viongozi kutumia majukwaa kama haya kuzungumza lakini kukosemaka kwa utekelezaji wa vitendo hivyo na kusababisha mikutano hii kutokuwa na mafanikio.

Mashirika hayo yametaka kuwepo kwa jitihada za pamoja za kujenga mifumo ya nishati mbadala na miundombinu ya umeme kwa kiwango ambacho kinanufaisha mamilioni ya Waafrika na kujikita katika kuzihimiza nchi nyingine kuchukua hatua zinazozuia ongezeko la joto duniani.

Licha ya hayo, serikali ya Kenya inaeleza kuwa inaendelea kutoa ufadhili unaohitajika kuimarisha nguvu za kijamii kukabili athari za mabadiliko ya hali ya hewa, na mishtuko mingine inayohusikana na mabadiliko ya hali ya hewa.

IMEANDALIWA NA KENNEDY WANDERA, SAUTI YA AMERIKA, NAIROBI.

Forum

XS
SM
MD
LG