Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 17:37

Rais Putin wa Russia ameshinda uchaguzi nchini mwake


Rais wa Russia, Vladimir Putin
Rais wa Russia, Vladimir Putin

Putin aliwaambia wafuasi wake anauchukulia uchaguzi huo ni wa kidemokrasia na kuwafuta kazi walioupinga

Rais wa Russia Vladimir Putin alisherehekea kushinda muhula mpya wa miaka sita baada ya uchaguzi ambao haukuwapa wapiga kura njia mbadala kutokana na vitisho au kufungwa jela kwa wapinzani wengi.

Putin aliwaambia wafuasi wake kwamba anauchukulia uchaguzi huo kuwa wa kidemokrasia na kuwafuta kazi wale waliopinga uchaguzi huo. Tuna kazi nyingi mbele yetu. Lakini tunapoimarishwa bila kujali nani anataka kututisha, kutukandamiza, hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa katika historia, hawajafanikiwa hivi sasa, na hawatafanikiwa katika siku zijazo, alisema Putin.

Uchaguzi huo wa siku tatu ulioanza Ijumaa na kuongeza utawala wa miaka 24 wa Putin ulifanyika katika mazingira ya udhibiti mkali ambapo ukosoaji wa umma kwa Putin au vita vyake nchini Ukraine haukuruhusiwa.

Matokeo kutoka tume kuu ya uchaguzi nchini Russia yalionyesha Putin alipata asilimia 87 ya kura. Shirika la habari la Reuters liliripoti mgombea wa kikomunisti Nikolai Kharitonov, alishika nafasi ya pili akiwa na chini ya asilimia 4 ya kura, mwanasiasa mgeni Vladislav Davankov alikuwa wa tatu, na Leonid Slutsky wa nne.

Forum

XS
SM
MD
LG