Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 12:02

Papa Francis hakutoa mahubiri jumapili ya matawi lakini aendelea na ibada

Papa Francis akisugua macho yake kabla ya kuanza kwa misa ya Jumapili ya Mitende kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatican, Jumapili, Machi 24, 2024. (Picha ya AP/Alessandra Tarantino)
Papa Francis akisugua macho yake kabla ya kuanza kwa misa ya Jumapili ya Mitende kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatican, Jumapili, Machi 24, 2024. (Picha ya AP/Alessandra Tarantino)

Papa Francis aliamua katika dakika za mwisho kutokwenda kuhubiri wakati wa Misa ya Jumapili ya matawi  katika Uwanja wa St.Peter  kuepuka hotuba ndefu mwanzoni mwa wiki takatifu yenye shughuli nyingi ambayo itaipa changamoto  afya yake inayozidi kuwa dhaifu.

Akiwa anasumbuliwa na magoti na matatizo ya kupumua yanayoendelea, Francis pia hakushiriki katika msafara wa makadinali kuzunguka mnara katika eneo la uwanja mwanzoni mwa Misa. Badala yake, Papa huyo mwenye umri wa miaka 87 alibariki matawi ya mitende na matawi ya mizeituni yaliyobebwa na waumini kutoka madhabahuni.

Francis alitarajiwa kutoa mahubiri katikati ya ibada na alikuwa ametangaza sala wakati wa Misa. Lakini baada ya kimya cha sekunde kadhaa, watangazaji walisema Francis ameamua kutotoa mahubiri yenyewe.

Maafisa wa Vatikani walikadiria watu wapatao 25,000 walihudhuria Misa hiyo, iliyofanyika chini ya anga ya jua, yenye upepo wa masika.

Forum

XS
SM
MD
LG