Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 07:08

O.J. Simpson afariki kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 76

O.J. Simpson
O.J. Simpson

Nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Marekani NFL  na mcheza filamu ambaye alifutiwa mashtaka ya mauaji ya mkewe na rafiki yake wa kiume katika kesi iliyoteka  Marekani  na dunia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

O.J. Simpson amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani, kwa mujibu wa taarifa ya familia yake kwenye akaunti yake ya X.

FILE - O.J. Simpson akionyesha furaha baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya vifo vya Nicole Brown Simpson na Ronald Goldman. Mawakili wake F. Lee Bailey, kushoto, na Johnnie L. Cochran Jr. wakiwa pamoja naye.(Myung J. Chun/Los Angeles Daily News via AP, Pool, File)

Gazeti la The Post lilisema kwamba alikufa siku ya Jumatano, akiwa amezungukwa na watoto wake na wajukuu.

Ingawa Simpson hakukutwa na hatia ya vifo vya Nicole Brown Simpson na Ronald Goldman, miaka mitatu baada ya kesi hiyo ya jinai alipatikana na hatia ya kuwajibika katika kesi ya madai iliyofunguliwa na familia za waathirika.

Forum

XS
SM
MD
LG