Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 13:54

Nigeria, Afrika Kusini na Jamaica zaandika historia katika kombe la Dunia la wanawake


Wendy Shongwe wa Afrika Kusini akisherehekea na bendera ya taifa lake baada ya mechi ya Kundi G ya Kombe la Dunia la kandanda ya Wanawake kati yao na Italia mjini Wellington, New Zealand, Agosti 2, 2023.
Wendy Shongwe wa Afrika Kusini akisherehekea na bendera ya taifa lake baada ya mechi ya Kundi G ya Kombe la Dunia la kandanda ya Wanawake kati yao na Italia mjini Wellington, New Zealand, Agosti 2, 2023.

Timu hizi zimefanikiwa kuingia raundi ya 16 ikiwa ni  kwa mara ya kwanza kwa Afrika Kusini na mara tatu kw Nigeria huku pia timu ya Afrika Kusini ikiandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza katika kombe la dunia

Timu za Afrika Kusini Banyana Banyana na timu ya Nigeria Super Falcons zimeandika historia nyingine kwa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia la wanawake huko New Zealand na Australia.

Timu hizi zimefanikiwa kuingia raundi ya 16 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Banyana Banyana huku pia timu hiyo ikiandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza katika kombe la dunia.

Na kwa upande wa Nigeria ambao wanashika namba 40 duniani wanaingia hatua hii kwa mara ya tatu katika historia yao. Nigeria wameweka matatizo yao pembeni ya kudai malipo na chama cha soka nchini kwao na kuvuka kwenye kundi gumu lililokuwamo bingwa wa Olimpiki Canada.

Nigeria pia wameweka rekodi ya kuvuka hatua ya makundi bila kupoteza hata mchezo mmoja kwa mara ya kwanza.

Timu ya Nigeria ina wachezaji kadhaa wenye vipaji ikiwa ni pamoja na washambuliaji kama vile Asisat Oshoala anayechezea Barcelona na Rasheedat Ajibade kutoka kikosi cha Atletico Madrid, lakini pia wanao mabeki wenye uwezo wa hali ya juu wasio na majina makubwa ambao wamezuia mechi mbili bila kufungwa bao lolote.

Ushindi huu unamaanisha kuwa mashindano haya yamepata ushindi mara nne kutoka kwa mataifa ya Afrika - mara mbili ya rekodi ya awali (1999, 2015 na 2019).

Katika raundi ya 16 Nigeria wanakutana na timu nambari tatu duniani Uingereza ambao wanapewa nafasi kubwa ya ushindi lakini hilo haliwatishi kikosi cha Super Falcons wa Nigeria.

Kwa upande mwingine timu ya Jamaica –Reggae Girls pia imeshangaza dunia ikiwa imecheza kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia la wanawake miaka minne iliyopita, na kupoteza michezo yote mitatu. Na sasa wameingia kwa mara ya pili na kuwatoa timu nambari 8 duniani Brazil na kwa mara kwanza kuingia raundi ya mtoano.

Forum

XS
SM
MD
LG