Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 14:01

Nchi nyingine kujiunga na BRICS


Rais wa China Xi Jinping akipunga mkono wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS uliofanyika Brazili, Novemba 13, 2019. Picha na REUTERS/Ueslei Marcelino.
Rais wa China Xi Jinping akipunga mkono wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS uliofanyika Brazili, Novemba 13, 2019. Picha na REUTERS/Ueslei Marcelino.

Viongozi wa Jumuiya ya nchi zinazoendelea haraka kiuchumi, BRICS - Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini – watakutana mjini Johannesburg kuanzia Jumanne hadi Alhamisi kwa mkutano wa kilele wa kila mwaka.

Suala la upanuzi wa jumuiya hiyo linatarajiwa kuwa juu kwenye ajenda ya mkutano huo.

Kimsingi, wanachama wa kundi hili hawana masilahi mengi ya pamoja. Brazil, India na Afrika Kusini ni nchi za kidemokrasia, wakati China na Russia zina utawala wa kimabavu. Hata hivyo, jambo moja ambalo wanakubaliana ni kutokuwa na imani na utaratibu wa kiuchumi duniani unaoongozwa na Marekani na kuwa na nia ya kuunda njia mbadala ambayo nchi za kusini mwa dunia zitakuwa na ushawishi mkubwa zaidi.

Jumuiya ya BRICS wachambuzi wanasema imeanza kupata umashuhuri wa haraka kutokana na idadi ya nchi zinazotaka kujiunga.

Takriban mataifa 40, ikiwa ni pamoja na Argentina, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, zimeeleza nia ya kujiunga na kundi hilo. Majadiliano kuhusu wanachama wapya huenda yakawa juu kwenye ajenda ya mkutano huo, wakati wanachama wa BRICS wakitofautiana kuhusu faida za upanuzi huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Ryabkov huko Tehran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Ryabkov huko Tehran.

Aidha, baadhi ya wachambuzi, pamoja na Jim O'Neill, mchumi wa zamani wa Goldman Sachs aliyebuni kifupi cha jina hilo la BRICS, wanasema kundi hilo halijapata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009. Mikatekiso Kubayi ambaye ni mtafiti katika Taasisi ya Majadiliano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini anapinga hoja hiyo.

"Kuna zaidi ya nchi 40 ambazo zimeeleza nia ya kujiunga na BRICS," Kubayi alisema. "Ni wazi nchi hizo zaidi ya 40 zimeona kitu, unajua, wanataka kujiunga na kundi hilo kwa kuwa kuna faida fulani au matumizi au thamani ya BRICS."

Na hivi ndivyo Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Naledi Pandor alisema wiki iliyopita.

"Muktadha wa sasa wa siasa za kimataifa umechochea nia mpya kutaka kujiunga na BRICS kama nchi zalizo kusini mwa dunia zinapotafuta njia mbadala katika dunia yenye mivutano mbali mbali."

Steven Gruzd, mchambuzi katika Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Afrika Kusini, alisema iwapo mataifa mengi yasiyo ya kidemokrasia yatajiunga inaweza kuufanya umoja huo kuwa na upinzani mkali zaidi dhidi ya nchi za Magharibi.

"Hakika, iwapo BRICS itapanuka na kujumuisha nchi kama Iran, hii bila shaka itaongeza sauti ya upinzani dhidi ya Magharibi, na mwelekeo wa majadiliano" alisema Gruzd.

Tayari, BRICS ina jumla ya asilimia 40 ya idadi ya watu wote duniani, na inakadiriwa kuwa na robo ya mapato jumla ya dunia. Katika suala la uwezo wa ununuzi, nchi za BRICS kwa sasa zina sehemu kubwa katika uchumi wa duniani kuliko nchi za G-7.

Forum

XS
SM
MD
LG