Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 14:02

Mtoto wa Gaddafi aachiwa huru Libya


Seif al-Islam Gaddafi
Seif al-Islam Gaddafi

Mwana wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, saif al-Islam ameripotiwa kuachiwa huru baada ya kuwa kizuizini kwa miaka sita.

Inaripotiwa kuwa kuachiwa kwake kutaleta mgogoro zaidi wa kisiasa na kiusalama nchini Libya.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari alikuwa akizuiliwa na kundi la wanamgambo katika mji wa Zintan kwa miaka sita.

Taarifa nchini Libya zinasema kuwa wanamgambo hao walimuachilia huru kufuatia ombi la serikali ya mpito nchini Libya.

Serikali hiyo inasemekana ilikuwa tayari imetoa msamaha kwa Saif al-Islam.

Hata hivyo, alikuwa amehukumiwa kifo na mahakama mjini Tripoli, magharibi mwa nchi hiyo bila yeye kuwepo mahakamani.

Maeneo ya magharibi yanatawaliwa na serikali inayopingana na serikali ya mashariki mwa Libya, lakini serikali hiyo ya magharibi yenye makao yake makuu Tripoli ndiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Taarifa zilizowahi kutolewa awali kuhusu kuachiliwa kwa Saif al-Islam Gaddafi baadaye zilibainika kuwa na uongo.

Mtoto wa Gaddafi pia anakabiliwa na tuhuma uhalifu dhidi ya binadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yenye makao yake mjini The Hague, Uholanzi.

XS
SM
MD
LG