Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 23:10

Mapigano kati ya koo yaua watu sita Somalia


Eneo la kati la Somalia
Eneo la kati la Somalia

Sio chini ya watu kumi wameuawa na wengine tisa kujeruhiwa wakati wanamgambo wa koo mbili hasimu kupambana katika eneo la kati la Somalia, wakazi na viongozi wa jamii wameeleza Jumamosi.

Wapiganaji hao ambao wanatokea katika koo ndogo za Air na Duduble walianza kupigana mapema Jumamosi asubuhi katika kijiji cha Labi-Aano, kilichopo kilometa 45 mashariki ya Dhuusamareeb. Mapigano hayo yalitokana na ugomvi na visasi vya koo.

“Mpaka sasa tumepata taarifa kuwa watu sita wameuawa katika ugomvi huo kati ya koo hizo na wengine zaidi ya tisa wamejeruhiwa,” Mohamed Ali Ilmi, gavana wa mkoa wa Galgudud ameiambia VOA kwa simu.

Lakini bado mpaka sasa eneo hilo linamachafuko. Kuna uwezekano kuwepo mapigano zaidi wakati matayarisho ya vita yakiendelea katika vijiji vya karibu,” amesema gavana.

Kwa upande wake Hassan Ali Omar, mzee mmoja katika mkoa huo amesema mapigano hayo yalianzishwa na uhasama wa muda mrefu uliokuwepo katika umiliki wa ardhi na malisho.

“Mapigano haya yamejirudia mara nyingi na yanafungamana na uhasama wa muda mrefu kati ya koo ndogo mbili. Tunasikitika kwamba yamesababisha vifo vya binadamu,” Omar amesema.

Mpigano haya ya hivi karibuni ya koo hizo yametokea wakati nchi ya Somalia inakabiliwa na janga la ukame mkubwa ambao umeendelea kulitumbukiza taifa hili dogo lenye kutegemea misaada katika dimbwi la baa kubwa la njaa.

XS
SM
MD
LG