Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 12:57

Morocco haitohudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini


Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita
Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita

Morocco bado haijawasilisha rasmi ombi la kujiunga na muungano wa BRICS na haitohudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, shirika la habari la serikali MAP limesema Jumamosi.

Ikinukuu chanzo cha kidiplomasia ambacho jina lake halikutajwa, MAP ilikanusha taarifa ya waziri wa Afrika Kusini wa mambo ya nje Anil Sooklal ambaye alisema mapema mwezi huu kwamba Morocco ni miongoni mwa mataifa yanayotaka kujiunga na BRICS.

“Afrika Kusini ilijipa mamlaka ya kuzungumza kuhusu uhusiano wa Morocco na BRICS bila mashauriano ya awali,” shirika la habari la MAP limesema.

Kundi hilo la mataifa yenye uchumi unaokuwa kwa kasi kwa sasa lina nchi wanachama -- Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, lakini uwezekano wa kulipanua kundi hilo utajadiliwa katika mkutano wake na Afrika Kusini ilisema zaidi ya nchi 40 zilionyesha nia ya kujiunga na BRICS.

Forum

XS
SM
MD
LG