Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 06:37

Mnara wa kumbukumbu ya Martin Luther King Jr wazinduliwa


Rais Barack Obama anazungumza wakati wa kuzindua mnara wa kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. mjini Washington, Oktoba 16, 2011.
Rais Barack Obama anazungumza wakati wa kuzindua mnara wa kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. mjini Washington, Oktoba 16, 2011.

Mnara wa Martin Luther King uliopewa jina la Jabali la Matumaini wazinduliwa Washington, DC

Rais wa Marekani Barack Obama Jumapili ameongoza sherehe za uzinduzi rasmi wa mnara wa kumbukumbu kwa heshima ya mtetezi wa haki za kiraia Martin Luther King Jr katika uwanja wa kitaifa jijini Washington DC.

Rais Obama ambaye ndiye rais wa kwanza mweusi nchini Marekani alitoa hotuba hiyo mbele ya maelfu ya watu na watetezi wa haki za kiraia pamoja na familia ya marehemu Martin Luther King Junior. Sherehe za hizo zimeandaliwa kwa heshima ya mshindi wa tuzo la amani la Nobeli Martin Luther King Jr ambaye alitetea haki za wote weupe kwa weusi hapa Marekani.

Mnara huo uliopewa jina la Jabali la Matumaini umegharimu dola milioni 120. Sherehe hizo awali zilitazamiwa kufanyika Agosti 28 lakini zikaahirishwa kutokana na kitisho cha kimbunga Irene. Mradi wa kutengeneza mnara huo wa Martin Luther King Jr ulichukua muda wa miaka 15 kukamilika. Siku hii ni ya kwanza katika uwanja wa kitaifa hapa Washington DC kuadhimishwa kwa heshima ya M’marekani mweusi.

XS
SM
MD
LG